Pages

Monday, February 10, 2014

Dk.ASHA ROSE MINGIRO NA KATIBA

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha Rose Migiro
SOURCE:Mwananchi Newspapers

Tume ya mabadiliko ya Katiba imetangaza Rasimu ya Katiba ambayo imetoa sura mpya ya muelekeo wa Taifa.Rasimu hiyo ilizinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam Juni tatu mwaka huu na Makamu wa Rais Dk, Mohamed Gharibu Bilali.
Baadhi ya mambo yaliyopendekezwa na kutoa sura mpya ya Taifa ni pamoja na kuwa na Serikali tatu, Spika wa Bunge kutokuwa Mbunge wala mwanachama wa chama cha siasa.
Mengine ni kuwepo na mgombea binafsi jambo ambalo litatoa fursa kwa wananchi kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Wakati wa uzinduzi wa rasimu hiyo wadau mbalimbali walijitokeza kuhudhuria sherehe za uzinduzi huo ambapo wapo waliyopongeza hatua hiyo na wengine kulalamika kwamba kuna baadhi ya mambo yameachwa.
Wagombea binafsi
Jambo kubwa ambalo lilifurahiwa na kuungwa mkono na watu wengi wakiwamo viongozi wa juu wa serikali na wa kimataifa kuruhusiwa kuwepo kwa mgombea binafsi.
Kwa mujibu wa Tume ya Katiba kupitia Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioa anasema Tume imeridhia kuwa na mgombea binafsi baada ya kuchambua maoni mengi yaliyotolewa na wananchi.
Hiyo inamaana kwamba kila Mtanzania atakuwa na haki ya msingi ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi anayo itaka ndani ya nchi.
Lakini jambo hilo liliungwa mkono na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha Rose Migiro ambaye naye alihudhuria sherehe za uzinduzi huo na kupata nafasi ya kutoa maoni yake kuhusu mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu hiyo. Dk Migiro anasema hatua hiyo ni nzuri na itasadia wananchi kupata fursa ya kushiriki kuomba nafasi za uongozi wanazozitaka.
Anasema jambo hilo litazidi kuimarisha demokrasia ya nchi na kwamba huu ndiyo wakati sahihi wa wananchi kushiriki kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wanazozitaka.
“Mimi nimevutiwa sana na Rasimu ya Katiba kuwapa nafasi wananchi kuweza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani hiyo itakuwa fursa nzuri kwao kuonyesha uwezo wao,” anasema Migiro.Anasema kitu kikubwa alichokuwa anakifikiri ni kwamba Tanzania itaweza kuandika historia ya kutengeneza Katiba kwa njia ya amani.
“Mimi nilipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nilikuwa nafikiria sana suala la Katiba. Kitu kikubwa ni kwamba Tanzania itaandika historia ya kutengeneza Katiba kwa njia ya amani.”
Dk Migiro anaeleza kuwa jambo hilo limefanikiwa na sasa Tanzania inaandika historia katika nchi za Afrika kwa kuwa na Katiba iliyowashirikisha wananchi na iliyoundwa kwa njia ya amani.

UKUMBI KWA AJILI YA BUNGE LA KATIBA SASA KUKAMILIKA

Source :Mwananchi Newspapers
DODOMA
Matengenezo yaliyotarajiwa ndani ya ukumbi wa bunge la Muungano ambao ndio utakaotumika kwa bunge la Katiba, yamekamilika na sasa ukumbi huo uko tayari kwa kazi inayotarajia kuanza Februari 18 mwaka huu.
Kukamilika kwa ukumbi huo kunaondoa hofu iliyoanza kutanda kuwa huenda bunge hilo lingesogezwa mbele kwa siku tatu kwani kulikuwa na mashaka kwa kazi hiyo.
Jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alitembelea ukumbi huo kwa mara ya mwisho na kujiridhisha katika maeneo muhimu yaliyokuwa yakifanyiwa marekebisho .
Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi huo, Lukuvi alisema tayari viti 676 vimeshafungwa pamoja vipaza sauti vyake ambavyo Rais Jakaya Kikwete alionyesha mashaka kama vingekamilika kwa wakati.
Februari Mosi, Rais Kikwete alipita kukagua ukumbi huo wakati akielekea mkoani Mbeya ambapo alionyesha kutokuridhika hasa akatilia mashaka katika eneo la vipaza sauti ambako alisema kuwa bado kulikuwa na kazi kubwa ya kufanya.
Hata hivyo, jana Lukuvi licha ya kushuhudia kuwa vimefungwa katika viti vyote, lakini alipotakiwa na waandishi kuwasha kwa majaribio, wajenzi wa ukumbi walizuia na kusema kitaalamu hakutakiwa kuwasha jana kwani kazi ilikuwa bado inaendelea.
Alisema kuwa Ofisi ya Bunge imeshatafuta kumbi nyingine nje ya bunge kwa ajili ya kufanyika mikutano ambayo itahitaji wajumbe zaidi ya 60.

WAT'S UP KATIKA PC

Sasa waweza kuchat na marafiki wako wa wat's up kwa kutumi computer yako unachohitaji kufanya ni;
1:download applicatin ya wat's up kutoka http://www.whatsapp.com/android/
2:iingize katika computer yako
3:fuata maelekezo watakayohitaji
GOOD LUCK!!!1

ONYO KWA KUEELEKEA KUELKEA UCHAGUZI WA URAIS 2015

Kamishna wa sekrtarieti ya tume ya maandalizi ya uchaguzi
Jaji msataafu.Salome Kaganda
 Suala la baadhi ya viongozi nchini kuanza kampeni za kuwania urais mwaka 2015 kwa kumwaga fedha ili kujijengea mazingira ya ushindi, limechukua sura mpya baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuanza kuwabana.
Habari zilizosikika masikioni kwa wengi
na baadaye kuthibitishwa na Kamishna wa Sekretarieti hiyo, Jaji Mstaafu Salome Kaganda, zinaeleza kuwa chombo hicho cha Serikali tayari kimewaita watu hao na kuwapa onyo baadhi yao wakiwamo mawaziri na wabunge walioanza kufanya kampeni.
Jaji Kaganda alisema kuwa waliwaita baadhi ya wanasiasa hao ambao wengi wana hadhi ya ubunge na kuwaonya kutokana na kubainika kwamba wanakiuka kanuni za maadili.
“Kwa upande wetu tumeshawaita baadhi, tulizungumza nao na kuwaonya kuhusu nyendo zao. Wapo waliotuelewa, naona wamekuwa kimya wakiendelea na shughuli zao nyingine za ujenzi wa taifa kwa nyadhifa walizonazo, ingawa pia wapo wengine tunasikia wanaendelea,” alisema Jaji Kaganda.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepanga kuwachukulia hatua baadhi ya makada wake wanaodaiwa kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula wiki hii alikaririwa akiwa mjini Morogoro akisema kwamba tayari wamefungua mafaili ya watu wenye mitandao ya kampeni akisema wanaitambua mitandao hiyo hadi ngazi za mikoa na wataishughulikia.
Alisema kuwa muda wa kampeni za urais, udiwani, ubunge haujafika, hivyo wanaofanya kampeni sasa wanakiuka Katiba na Kanuni.
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alipoulizwa kuhusu hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaodaiwa kujipitisha kabla ya muda wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, alisema ofisi yake ipo tayari kuwashughulikia kwa mujibu wa utaratibu, ikiwamo kuwashtaki kwenye Sekretarieti ya Maadili, iwapo barua za malalamiko zitafikishwa kwake.
“Kwa jambo hili hatuwezi kuchukua hatua yoyote kama hakuna barua ya malalamiko iliyoletwa kwetu, hasa na vyama husika. Hivi sasa na sisi tumebaki tunaona na kusikia tu kwenye vyombo vya habari,” alisema Jaji Mutungi.
Wiki iliyopita wabunge wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokuwa kwenye ziara kwenye Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili, walihoji jinsi chombo hicho cha umma kilivyojipanga kuwashughulikia viongozi wanaodaiwa kumwaga fedha wakiwa katika maandalizi ya kugombea urais na ubunge.Mjumbe wa Kamati hiyo, Nyambari Nyangwine ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, alitaka kujua jinsi Sekretarieti hiyo, inavyoweza kuwashughulikia viongozi hao kwa kuwa vitendo hivyo vinakiuka maadili ya uongozi.
Kulingana na gazeti la Mwananchi la tarehe 11/02, Wabunge wawili, mmoja wa CCM na mwingine wa Chadema, jana walikula vichapo walipokuwa katika harakati za uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika katika kata 27 nchini.
Wabunge hao, Godbless Lema (Chadema) wa Arusha na Mchungaji Jackson Mwanjele wa Mbeya Vijijini walipata vipigo katika matukio tofauti yanayohusiana na uchaguzi huo.
Lema alidai kuwa alinusurika kifo kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa polisi na ilibidi aanguke chini na kujifanya amezirai ili kujiokoa, katika tukio lililotokea jana jioni, eneo la Shule ya Sombetini alipokuwa akielekea katika kituo cha kupigia kura.
Mara baada ya kufika jirani na kituo cha Sombetini, inadaiwa kuwa polisi walisimamisha gari ya Lema na kuanza kumuhoji lakini ghafla ilitokea kutoelewana kipigo kuanza. Katika tukio hilo, Lema alipata kipigo hadi kuangukia katika mfereji na akiwa chini, alionekana kama amezimia hivyo polisi walimuachia na kuokolewa na wafuasi wa Chadema.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Lema alisema bila kujifanya amezirai angeweza kuuawa... “Wamenipiga sijui kosa langu, mimi kama mbunge niliitwa na mawakala wakiomba gari kubeba masanduku na ni kweli nilikuwa nimewasha taa za gari nikishangilia. Kesho naenda kupimwa hospitali kwani nina maumivu kwenye mbavu. Baada ya hapo nitajua cha kufanya kwani walionipiga nawajua.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana jana kuelezea tukio hilo lakini mmoja wa polisi waliokuwa eneo la vurugu hizo, alisema walilazimika kimdhibiti Lema, kwani alikuwa anafanya fujo jirani na kituo cha kura.
“Hakuna aliyempiga, alianguka mwenyewe kwenye mfereji, tulimtaka aondoke kwa amani akagoma,” alisema askari huyo.

MOHAMED DEWJI NA JANUARY MAKAMBA WATAJWA KUWA KATI WATU WENYE NGUVU BARANI AFRIKA KWA MWAKA 2014.

Mohammed Dewji mwenye umri wa miaka 39 ametajwa kuwa kati ya watu mashuhuri barani Afrika ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani  $500 kulingana na jarida la forbes africa la hivi karibuni.
Mohammed Dewji
C.E.O of  Mohammed Enterprices (T) LTD

Bwana Dewji ni mwendelezaji wa biashara ya familia yao inayojulikana kwa kama(mohammed enterprises (T) Limited) ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa hapa nchini . Viwanda vya kampuni hii vimeajiri watu takriban 2500 kote nchini na kulingana na mwenyewe Dewji anasema kuwa kampuni hii inaingiza mapato ya dola za kimarekani bil.1.2 kwa mwaka. Vilevile Bw.Dewji amekuwa mbunge wa bunge tukufu la tanzania toka mwaka 2005.


January Makamba pia ni mmoja kati ya watanzania waliotajwa katika jarida la Forbse africa.
Vilevile January ni mmoja kati ya watu waliotjwa kuwa ni moja ya viongozi wadogo wa mwaka 2012 (Young globa Leaders). Kwa sasa januari ni waziri wa mawasiliano , sayansi na teknolojia. January Makamba ni mtoto wa mwanasiasa mashuhuri hapa nchini, Mzee Yusuf
Makamba.

Mr.January Makamba
Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia