Pages

Monday, February 10, 2014

ONYO KWA KUEELEKEA KUELKEA UCHAGUZI WA URAIS 2015

Kamishna wa sekrtarieti ya tume ya maandalizi ya uchaguzi
Jaji msataafu.Salome Kaganda
 Suala la baadhi ya viongozi nchini kuanza kampeni za kuwania urais mwaka 2015 kwa kumwaga fedha ili kujijengea mazingira ya ushindi, limechukua sura mpya baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuanza kuwabana.
Habari zilizosikika masikioni kwa wengi
na baadaye kuthibitishwa na Kamishna wa Sekretarieti hiyo, Jaji Mstaafu Salome Kaganda, zinaeleza kuwa chombo hicho cha Serikali tayari kimewaita watu hao na kuwapa onyo baadhi yao wakiwamo mawaziri na wabunge walioanza kufanya kampeni.
Jaji Kaganda alisema kuwa waliwaita baadhi ya wanasiasa hao ambao wengi wana hadhi ya ubunge na kuwaonya kutokana na kubainika kwamba wanakiuka kanuni za maadili.
“Kwa upande wetu tumeshawaita baadhi, tulizungumza nao na kuwaonya kuhusu nyendo zao. Wapo waliotuelewa, naona wamekuwa kimya wakiendelea na shughuli zao nyingine za ujenzi wa taifa kwa nyadhifa walizonazo, ingawa pia wapo wengine tunasikia wanaendelea,” alisema Jaji Kaganda.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepanga kuwachukulia hatua baadhi ya makada wake wanaodaiwa kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula wiki hii alikaririwa akiwa mjini Morogoro akisema kwamba tayari wamefungua mafaili ya watu wenye mitandao ya kampeni akisema wanaitambua mitandao hiyo hadi ngazi za mikoa na wataishughulikia.
Alisema kuwa muda wa kampeni za urais, udiwani, ubunge haujafika, hivyo wanaofanya kampeni sasa wanakiuka Katiba na Kanuni.
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alipoulizwa kuhusu hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaodaiwa kujipitisha kabla ya muda wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, alisema ofisi yake ipo tayari kuwashughulikia kwa mujibu wa utaratibu, ikiwamo kuwashtaki kwenye Sekretarieti ya Maadili, iwapo barua za malalamiko zitafikishwa kwake.
“Kwa jambo hili hatuwezi kuchukua hatua yoyote kama hakuna barua ya malalamiko iliyoletwa kwetu, hasa na vyama husika. Hivi sasa na sisi tumebaki tunaona na kusikia tu kwenye vyombo vya habari,” alisema Jaji Mutungi.
Wiki iliyopita wabunge wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokuwa kwenye ziara kwenye Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili, walihoji jinsi chombo hicho cha umma kilivyojipanga kuwashughulikia viongozi wanaodaiwa kumwaga fedha wakiwa katika maandalizi ya kugombea urais na ubunge.Mjumbe wa Kamati hiyo, Nyambari Nyangwine ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, alitaka kujua jinsi Sekretarieti hiyo, inavyoweza kuwashughulikia viongozi hao kwa kuwa vitendo hivyo vinakiuka maadili ya uongozi.

No comments: