Pages

Sunday, February 9, 2014

UKANUSHWA KUHUSU WATANZANIA WALIOKAMATWA NA MADAWA NCHINI CHINA KUNYONGWA

 Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imekanusha madai kuwa Watanzania 160 wamenyongwa nchini China baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa:
Benard Membe
“...habari za uhakika kutoka China zinasema Watanzania wenzetu 160 wamenyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya,” ilisema taarifa katika mtandao.
Hata hivyo, Mkubwa alisema hadi kufikia Julai mosi mwaka jana, idadi ya Watanzania waliokuwa wanatuhumiwa kwa makosa hayo huko China ilikuwa176. 
Alisema hata kama ingekuwa wamethibitika kutenda makosa na kuhukumiwa kifo, ingekuwa rahisi watu 160 kunyongwa kwa wakati mmoja.
“Inawezekana........

Waziri. James Limbeli
Tunaipongeza jumuiya ya kimataifa kwa kuungana na Tanzania katika vita yake dhidi ya ujangili ambao umewaangamiza wanyamapori, wakiwamo tembo kwa kiasi kikubwa. Takwimu za hivi karibuni, kwa mfano zimeonyesha kwamba iwapo kasi ya kuua tembo isipodhibitiwa sasa, Tanzania itakuwa haina tembo hata mmoja katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Takwimu hizo zinatisha na zinaonyesha jinsi Serikali ilivyoshindwa kulinda wanyamapori na badala yake ikajisalimisha kwa majangili kwa kuyaacha kufanya yanavyotaka. Sasa tumeambiwa kuwa, kwa upande wa jumuiya ya kimataifa juhudi za kusaidia vita hiyo itakayotumia mikakati ya muda mrefu na ya mpito zitaongozwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) na kuhusisha Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Benki ya Dunia (WB) na nchi za Uingereza, Marekani, Japan, Ujerumani, China, Ufaransa na Hispania.
Hatua ya jumuiya hiyo kuunga mkono vita hiyo imekuja baada ya Serikali kutangaza kwamba awamu ya pili ya ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’ itaanza wakati wowote. Hii ni baada ya operesheni ya awali kusitishwa Oktoba 31, mwaka uliopita kutokana na kukumbwa na kashfa ya vitendo vya kikatili dhidi ya raia, ambapo wananchi waliteswa, kuuawa na mali zao kuteketezwa na baadhi ya askari waliokuwa wakiendesha operesheni hiyo. Serikali imesema katika kipindi cha miezi mitatu hivi ambacho operesheni ya awali ilikuwa imesitishwa, vitendo vya ujangili vilipamba moto, ambapo wanyamapori wengi, hasa tembo waliteketezwa.
Awamu hiyo ya kwanza pia ilihusisha baadhi ya taasisi za kimataifa, ukiwamo Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WFP). Hata hivyo, ulikuwapo usiri mkubwa kuhusu matumizi ya fedha kutokana na vyanzo vya ndani, ikiwamo Serikali yenyewe kwa upande mmoja, na mchango uliotolewa na taasisi za kimataifa kwa upande mwingine. Zilikuwapo tuhuma za ubadhirifu wa fedha hizo, kwa maana ya matumizi yaliyokuwa nje ya malengo yaliyokusudiwa.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilithibitisha mwanzoni mwa wiki kuwa, askari zaidi ya 2,000 kutoka vyombo vya ulinzi na usalama walioshiriki katika operesheni hiyo ya awali hawajalipwa fedha zao na kwamba madai yao yamekuwa yakipigwa danadana kila kukicha, wakati zilikuwa zimetengwa Sh3.5 ambazo zilitosha kwa kazi hiyo. Pamoja na kukiri kutowalipa askari hao, Serikali imetoa kioja cha mwaka kwa kusema askari hao watalipwa kabla ya kuanza kwa awamu ya pili ya operesheni hiyo, kauli inayoweza kutafsiriwa kwamba fedha za awamu iliyopita zilitafunwa, hivyo askari hao sasa watalipwa baada ya kupatikana fedha za kuendesha awamu ijayo.
Hoja yetu ya msingi hapa ni kuwa, ili vita dhidi ya ujangili iwe endelevu lazima uwepo uwazi na uwajibikaji siyo tu katika utekelezaji wake, bali pia katika matumizi ya fedha na rasilimali zilizotengwa kwa ajili hiyo. Walipakodi wanayo haki ya kupata mchanganuo wa fedha zilizotumika katika utekelezaji wa operesheni iliyopita na inayotarajiwa kuanza hivi punde.
Haiingii akilini hata kidogo, kwa mfano kuona fedha zilizotengwa kuwalipa askari waliotekeleza operesheni hiyo zikitafunwa na waroho wachache serikalini na Serikali yenyewe kwa makusudi inashindwa kuwawajibisha. Ndiyo maana tunaitaka ihakikishe makosa yaliyofanyika katika operesheni iliyopita hayarudiwi, ingawa pia tunatarajia kwamba itawachukulia hatua wote waliohusika kuihujumu operesheni hiyo kwa namna moja ama nyingine.