Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imekanusha madai kuwa Watanzania 160 wamenyongwa nchini China baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.
![]() |
| Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa: Benard Membe |
Hata hivyo, Mkubwa alisema hadi kufikia Julai mosi mwaka jana, idadi ya Watanzania waliokuwa wanatuhumiwa kwa makosa hayo huko China ilikuwa176.
Alisema hata kama ingekuwa wamethibitika kutenda makosa na kuhukumiwa kifo, ingekuwa rahisi watu 160 kunyongwa kwa wakati mmoja.
Alisema hata hivyo, Serikali kupitia ubalozi wake nchini China, itafuatilia ili kufahamu kinachoendelea dhidi ya watuhumiwa wa kusafirisha dawa za kulevya nchini humo.
Pia alifafanua kuwa Tanzania haina mkataba na China kuhusu kubadilishana wafungwa,na kwamba watakaotiwa hatiani kwa vyovyote watanyongwa hadi kufa. kulingana sheria za nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment